Sudan Kusini kuwarudisha makwao wahamiaji kutoka Marekani
12 Septemba 2025
Matangazo
Kulingana na msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Sudan Kusini,Apuk Ayuel Mayen, wizara hiyo iko katika majadiliano na nchi walikotokea wahamiaji hao ili kuwarejesha makwao.
Sudan Kusini iliwapokea wahamiaji wanane kutoka Marekani mnamo mwezi Julai.Wahamiaji hao walikuwa wamefungwa kwa makosa makubwa ya uhalifu ila ni mmoja tu miongoni mwao aliyekuwa raia wa Sudan Kusini.
Rais Donald Trump ameipa kipaumbele hatua ya kuwaondoa nchini humo wahamiaji wasio na vibali na kuwarejesha makwao au katika nchi maskini.