Sudan: Maendeleo katika mapatano ya amani.
21 Desemba 2003Matangazo
NAIROBI: Zile juhudi za kuvimaliza vita vya ndani vinavyoendelea kudumu miaka 20 nchini Sudan zimeweza kupiga hatua muhimu mbele. Wawakilishi wa serikali ya Sudan na Jeshi la Kupigania Ukombozi wa Sudan, SPLA waliwafikiana katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi kugawanya mapato yanayotokana na uzalishaji wa mafuta, alithibitisha mpatanishi wa Kenya Lazaro Sumbeiywo. Swali la mgawanyo wa mapato ya mafuta lilikuwa kiini cha mivutano mikali kabisa kati ya serikali ya Khartoum na Chama cha Ukomobozi wa Sudan, SPLA. Hata hivyo pande hizo mbili hazikuweza bado kuwafikiana juu ya mgawanyo wa madaraka katika majimbo mbali mbali ya Sudan.
