Sudan-mazungumzo ya amani:
12 Desemba 2003Matangazo
Geneva: Waziri wa habari wa Sudan Elzahwi Ibrahim Malik amesema kwamba serikali na waasi wa SPLA nchini humo wanaendelea vizuri na mazungumzo yao ya amani na kwamba mkataba wa mwisho utafikiwa kabla ya mwezi Januari mwakani. Bw Malik alikua akizungumza na waandishi habari mjini Geneva , kandoni mwa mkutano wa kilele wa kimataifa wa habari na mawasiliano. Ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa isaidie kupatikana utulivu wa kudumu nchini Sudan pamoja na msaada katika miradi ya maendeleo. Mazungumzo hayo ya amani kati ya serikali ya Khartoum na SPLA yanaendelea nchini Kenya.
