Sudan na Iran zarejelea uhusiano wa kidiplomasia
10 Oktoba 2023Katika taarifa iliyochapishwa mtandaoni, wizara ya mambo ya nje ya Sudan, imesema kuwa mataifa hayo mawili yamekubaliana kuchukuwa hatua zinazohitajika kufungua balozi zao katika nchi hizo hivi karibuni.
Iran na Sudan kuimarisha ushirikiano
Shirika la habari la serikali ya Iran, limeripoti kuwa pande hizo mbili zilikubaliana kuimarisha ushirikiano katika nyanja tofauti ambao unaweza kutimiza maslahi ya mataifa hayo mawili na kuhakikisha usalama na utulivu katika kanda hiyo.
Viongozi wa mataifa hayo mawili walikutana Baku
Waziri wa mambo ya nje wa Iran Hossein Amir-Abdollahian, na mwenzake wa Sudan, Ali al-Sadiq, walikutana mjini Baku nchini Azerbaijani mwezi Julai, huu ukiwa mkutano wa kwanza unaojulikana wa maafisa wakuu wa mataifa hayo mawili tangu mwaka 2016.