1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Sudan yaanza utekelezaji wa usitishwaji mapigano

18 Juni 2023

Pande zinazohasimiana nchini Sudan zimeanza utekelezaji wa makubaliano ya kusitisha mapigano baada ya miezi miwili ya mapambano.

Sudan Khartoum | Mgogoro
Moshi unaonekana kwa mbali mjini KhartoumPicha: AFP/Getty Images

Pande zinazohasimiana nchini Sudan zimeanza utekelezaji wa makubaliano ya kusitisha mapigano baada ya miezi miwili ya mapambano yaliyolitumbukiza taifa hilo kwenye machafuko.

Wakaazi katika mji mkuu Khartoum na mji jirani wa Omdurman wamesema kumekuwepo na utulivu katika masaa ya awali ya makubaliano hayo mapema hii leo, baada ya mapigano makali yaliyoripotiwa jana Jumamosi.

Makubaliano hayo ya siku tatu yamefikiwa kabla ya mkutano wa Umoja wa Mataifa na mataifa mengine wa kuomba ufadhili kwa ajili ya misaada ya kiutu huko nchini Sudan utakaofanyika kesho Jumatatu.Watoto milioni 1 wameachwa bila makao katika mapigano Sudan

Umoja huo umesema ulipokea chini ya asilimia 16 ya dola bilioni 2.57 zinazohitajika kusaidia wenye mahitaji nchini Sudan kwa mwaka huu 2023, lakini bado inahitaji dola milioni 47 zaidi za msaada kwa wakimbizi katika eneo la Pembe ya Afrika.