1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sudan yafungua tena anga lake

15 Januari 2020

Kiongozi wa Baraza la uongozi nchini Sudan amesema nchini hiyo imelifungua tena  anga  lake, wakati  jeshi likitangaza kuwa wanajeshi wawili wameuwawa  na wengine  wanne  wamejeruhiwa wakati  wa  kuzima  uasi.

Sudan Abdel Fattah al-Burhan, Chairman Transitional Military Council (TMC)
Picha: Imago Images/Xinhua

Ghasia  hizo  zilikuwa  makabiliano  makubwa  kuwahi kufanyika  kati ya  maafisa  hao wa  zamani  wa  usalama na  waungaji  mkono  wa  utawala  mpya, ambao ulisaidia kumuangusha  kutoka  madarakani  Bashir  mwezi  Aprili baada  ya  miaka  30  akiwa  madarakani.  Kiongozi wa baraza la  mpito Luteni Jenerali Abdel Fattah al-Burhan amesema jeshi la nchi hiyo linaudhibiti wa  majengo  yote ya idara  ya  usalama  wa  taifa.

Katika  hotuba  mapema  leo, kiongozi  wa  baraza linaloongoza  nchi  hiyo, luteni  jenerali  Abdel Fattah al-Burhan, aliapa  kutoruhusu  mapinduzi yoyote kutokea nchini humo. Maafisa  wa  zamani  wa  usalama  wa  taifa walipambana  katika  mji  mkuu Khartoum, kwa  masaa kadhaa  hadi  pale  majeshi  ya  serikali  yalipozima uasi huo  jioni ya  jana, kulingana na wakaazi  na  duru  za kijeshi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW