1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sudan yakubali upatanishi wa S.Kusini majimbo ya mpakani

5 Novemba 2018

Sudan kwa mara ya kwanza imekubali upatanishi wa Kiongozi wa Sudan Kusini, wa mazungumzo ya amani kuhusu mvutano juu ya maeneo ya mpaka ya kordofan kusini na Blue Nile. Sudan imesema amani ni chaguo la kimkakati.

Südsudan, Juba: Rebellenführer Machar zurück im Südsudan
Picha: picture-alliance/dpa/B. Chol

Sudan iliwahi kuilaumu Sudan Kusini kwa kuchochea machafuko katika mikoa  hiyo miwili ambako  waasi wanapigana dhidi ya utawala wa serikali ya Sudan baada ya sehemu kubwa ya  ardhi ya majimbo hayo kuwa sehemu ya  Sudan Kusini  huru katika mwakan  2011.

Serikali ya Sudan imetangaza usitishaji mapigano wa upande mmoja katika majimbo yote mawili na pia katika jimbo lenye mgogoro la Darfur magharibi mwa Sudan tangu mwaka 2015, na sasa mapigano yamepungua.

Msemaji wa chama tawala nchini Sudan  Ibrahim al-Sadiq alisema, rais Salva Kirr wa Sudan Kusini ameanza mazungumzo na makundi ya  chama cha Sudan Peoples Liberation Army-SPLM yalioko katika mikoa hiyo miwili kuhusu  suluhisho la amani.

Ramani ya Sudan na Sudan Kusini ikionyesha majimbo yenye mizozo ya Blue Nile na Kordofan.

Alisema mazungumzo hayo chini ya udhamini  kwa udhamini wa Umoja wa Afrika yanatarajiwa kuanza mjini Addis ababa katikati ya mwezi ujao wa Desemba.

"Amani ni chaguo la kimkakati kwa serikali ya Sudan na kwa hivyo serikali imeidhinisha upatanishi wa rais wa Sudan Kusini Salva Kiir," alisema Sadiq.

Maelfu yawatu wameuawa katika vita vya wenyewe kwa wenyewe vya mataifa ya Sudan, ikiwemo jimboni Darfur, ambako waasi wamekuwa wakipigana dhidi ya serikali ya Rais Omar Hassan al-Bashir tangu mwaka 2003.

Serikali ya Kiir na kundi kuu la waasi wa Sudan Kusini walisaini makubaliano ya amani mwezi Spetemba mjini Khartoum, yakinuwia kukomesha vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoiharibu nchi hiyo tangu mwaka 2013.

Mwandishi: Iddi Ssessanga

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW