1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sudan yaongeza muda wa kukifungua kivuko cha Adre

Sylvia Mwehozi
14 Novemba 2024

Mamlaka nchini Sudan zimeongeza muda wa kukifungua kivuko muhimu cha usambazaji wa misaada ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa kwa miezi mitatu zaidi.

Mpaka wa Adre
Watu wakikimbia Magharibi mwa Darfur kuelekea ChadPicha: Zohra Bensemra/REUTERS

Mamlaka nchini Sudan zimeongeza muda wa kukifungua kivuko muhimu cha usambazaji wa misaada ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa kwa miezi mitatu zaidi.

Kivuko hicho cha Adre, kinachounganisha nchi jirani ya Chad na jimbo la Darfur, kilifunguliwa kwa mara ya kwanza katikati ya mwezi Agosti.Mpango wa Chakula, WFP waomba utulivu nchini Sudan ili litoe huduma zake

Sudan imekumbwa na mzozo mbaya tangu Aprili 2023 kati ya jeshi linaloongozwa na Abdel Fattah al-Burhan, na kundi la wanamgambo wa RSF, chini ya mshirika wake wa zamani Mohamed Hamdan Daglo.

Mapigano yamepamba moto katika wiki za hivi karibuni katika mzozo ambao tayari umesababisha maelfu ya watu kuuawa na zaidi ya milioni 11 kukimbia makazi yao.

Katika kikao cha Baraza la Usalama mjumbe wa Umoja wa Mataifa wa Sudan Al-Harith Idriss Mohamed aliishutumu RSF kwa kusafirisha silaha na zana za kivita kupitia kivuko cha Adre.

 

 

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW