1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sudan yaongoza tena orodha ya Shirika la IRC

16 Desemba 2025

Sudan kwa mara nyingine tena imeongoza orodha ya waangalizi wa kimataifa wa migogoro ya kibinadamu iliyotolewa na Shirika la Kimataifa la Misaada ya Kiutu la International Rescue Committee (IRC).

Sudan Tawila 2025 | wakimbizi wa ndani
Familia za wakimbizi wa ndani nchini Sudan katika kambi ya wakimbizi ya el-Fasher nchini humo mnamo Oktoba 31,2025Picha: NRC/AP Photo/picture alliance

Katifa taarifa, mkuu wa IRC  David Miliband , amesema kile shirika hilo limekiona kwenye mitaa na vijiji vya nchi hiyo siyo jambo la bahati mbaya na kwamba ulimwengu haushindwi kushughulikia tu mzozo huo bali matendo na maneno yanarefusha na kuuzawadia mzozo huo.

Miliband amesema ukubwa wa mgogoro nchini Sudan, unaoshikilia nafasi ya kwanza katika orodha ya shirika hilo kwa mwaka wa tatu mfululizo na ambao sasa ndio mgogoro mkubwa zaidi kurekodiwa, ni ishara ya mparaganyiko unaoshuhudiwa kote ulimwenguni.

Orodha hiyo inaangazia nchi 20 ambazo zinakabiliwa na hatari zaidi ya dharura mpya au mbaya zaidi za kibinadamu.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW