MigogoroSudan
Sudan yasitisha mahusiano na IGAD kufuatia mwaliko wa Daglo
17 Januari 2024Matangazo
Taarifa iliyotolewa na wizara ya mambo ya kigeni ya Sudan, imesema uamuzi wa IGAD wa kumkaribisha kiongozi wa kikosi cha RSF, Mohammed Hamdan Daglo, kuhudhuria mkutano wa kilele wa jumuiya hiyo utakaofanyika kesho Alhamisi ni "ukiukaji mkubwa wa hadhi na uhuru" wa taifa hilo.
Hadi sasa Jumuiya hiyo haijatoa majibu yoyote kuhusu tuhuma hizo wala kuthibitisha mwaliko wa Daglo kwenye mkutano huo wa kilele wa 42 utakaofanyika mjini Kampala nchini Uganda.
Jumuiya ya IGAD yenye mataifa nane wanachama imekuwa ikiongoza juhudi za kikanda kuutafutia suluhu mzozo wa Sudan uliozuka April mwaka jana.