Sudan yataka mjumbe wa UN kuondolewa
27 Mei 2023Hatua hii ya Jenerali Burhan inachukuliwa katikati ya mzozo unaoendelea nchini humo kati yake na aliyewahi kuwa msaidizi wake jenerali Mohammed Hamdani Dagalo.
Msemaji wa Guterres, Stephane Dujarric amesema kiongozi huyo ameshtushwa na ombi la kubadilishwa kwa mjumbe huyo, ambaye kulingana naye anafanya kazi nzuri kama mwakilishi wake.
Perthes na ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo wamekuwa wakilengwa na waandamanaji wanaounga mkono jeshi ambao mara kwa mara wamekuwa wakimshutumu kwa uingiliaji wa kigeni na kutaka aondolewe.
Hii na hatua ya karibuni, katika msururu wa hatua zinazochukuliwa na mkuu huyo wa majeshi, ambaye wiki iliyopita alimfuta rasmi wadhifa wa umakamu, mpinzani wake Mohammed Hamdan Dagalo katika baraza tawala.
Soma Zaidi:Marekani, Saudia wasema usitishwaji mapigano Sudan unaheshimiwa kwa kiwango fulani