SUMATRA: Yahofiwa kuzuka kwa malaria Indonesia.
8 Aprili 2005Matangazo
Kundi la watalaamu wa matibabu limeonya uwezekano wa kuzuka kwa mkurupuko wa homa ya malaria katika pwani ya Sumatra nchini Indonesia kufuatia tetemeko kubwa la ardhi siku chache zilizopita.
Baadhi ya visiwa katika pwani ya Sumatra vimedidimia chini ya vipimo vya usawa wa bahari kufuatia tetemeko hilo na kusababisha vidimbwi vya maji vilivyo geuka kuwa makao ya mbu wenye viini vya ugonjwa wa malaria.
Madaktari hao wameitaka serikali ya Indonesia kutia bidii ya kunyunyiza madawa ili kuwakinga raia wake kutokana na maambukizo ya malaria.