1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiUingereza

Sunak amtakia afua Mfalme Charles III anayeugua saratani

6 Februari 2024

Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak amesema "ameshtushwa na kuhuzunishwa" na taarifa za mfalme Charles III kugunduliwa kuwa na saratani.

Uingereza | Mfalme Charles III.
Tangazo la Mfalme Charles III wa Uingereza kugundulika kuwa na saratani lilitolewa siku ya Jumatatu, Februari, 02, 2024Picha: Victoria Jones/empics/picture alliance

Sunak ameliambia shirika la habari la BBC kuwa, kwa upande mwengine anashukuru kwamba ugonjwa huo umegunduliwa mapema na kuongeza kuwa mfalme huyo yupo kwenye maombi ya wengi.

Kasri la Buckingham jana jioni lilitangaza kuwa mfalme Charles ameanza matibabu  kwa aina ya saratani ambayo bado haijawekwa wazi. Saratani hiyo sio ya tezi dume lakini imegunduliwa wakati akipokea matibabu ya uvimbe katika tezi dume.

Chini ya miezi 18 ya utawala wake, mfalme Charles mwenye umri wa miaka 75 amesimamisha shughuli zake za umma japo ataendelea na shughuli za serikali ikiwemo mikutano ya kila wiki na waziri mkuu.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW