1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sunak na Scholz kukutana mjini Berlin

24 Aprili 2024

Waziri mkuu wa Uingereza Rishi Sunak anatarajiwa kufanya mazungumzo na Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz, katika ziara yake ya kwanza mjini Berlin tangu kushika nafasi yake hiyo miezi 18 iliyopita.

Rishi Sunak
Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak Picha: Benjamin Cremel/Pool via REUTERS

Rishi Sunak Sunak analenga kuzungumzia masuala mbalimbali ikiwemo ulinzi na usalama barani Ulaya.

Viongozi hao wanatarajiwa kujadiliana pia kuhusu Ukraine, viwango vya matumizi ya ulinzi, na msukumo wa Ujerumani wa kuimarisha ulinzi wa anga wa Jumuiya ya kujihami ya NATO barani Ulaya katikati mwa mashambulizi ya makombora ya Urusi dhidi ya Ukraine.

Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak kukutana na Kansela Scholz nchini Ujerumani

Ziara ya Sunak mjini Berlin inajiri baada ya kutembelea mji mkuu wa Poland, Warsaw ambapo aliahidi kuongeza hatua kwa hatua matumizi ya ulinzi ya Uingereza hadi asilimia 2.5 ya Pato la Taifa ifikapo 2030.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW