1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUingereza

Sunak, Starmer wakabiliana katika mdahalo wa Uingereza

27 Juni 2024

Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak na kiongozi wa chama cha Labour Keir Starmer walikabiliana ana kwa ana Jumatano usiku katika mdahalo wao wa mwisho kabla ya uchaguzi wa wiki ijayo.

Sunak na Starmer katika mdahalo wa uchaguzi
Utafiti wa maoni wa YouGov ulisema mdahalo huo ulitoka sare, kila mmoja akipata asilimia 50.Picha: Jonathan Hordle/ITV via Getty Images

Viongozi hao wawili walishambuliana vikali kuhusu uaminifu wao na wa vyama vyao. Huku chama cha Conservative cha Sunak kikiwa nyuma ya chama cha Labourkwa karibu pointi 20 kwenye utafiti wa maoni, waziri mkuu huyo alishambulia Starmer akimtuhumu kwa kutokuwa mkweli kwa nchi kuhusu uhamiaji, kodi na haki za wanawake, na akawahimiza wapiga kura kutojisalimisha kwa chama cha Labour.

Starmer alijibu kuwa Sunak ni tajiri mno kiasi kwamba hawezi kuelewa maswala ya Waingereza wengi wa kawaida. Utafiti wa haraka wa maoni uliofanywa na shirika la YouGov ulisema kuwa mdahalo huo ulitoka sare, kila mmoja akipata asilimia 50. Utafiti wa maoni unaonesha kuwa Starmer wa Labour anaelekea kushinda uchaguzi kwa wingi mkubwa wa kura, na kuufikisha tamani utawala wa Conservative wa miaka 14.