1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SURA YA UJERUMANI:UJERUMANI DOLA LA 4 USONI KUUZA MAZAO YA KILIMO DUNIANI.

Ramadhan Ali28 Januari 2005

Kwa kweli,hali za wakulima wa Ujerumani wakati huu si nzuri na hii yafaa kuungama na inafahamika.Kwani,uvunaji mazao ya kilimo kupita kiasi na mahitaji ya soko na hivyo kuporomoka kwa bei za mazao hayo ni matatizo yao yaliopo sasa.

Kwa upande mwengine, kwa mara ya kwanza tangu kupita miaka 3 faida ya viwanda vya kilimo vya wakulima imeanza kupanda tena.Na hii inatokana hasa na kuongezeka kwa bidhaa ambazo Ujerumani inauza nchi za n’gambo kutoka sekta ya kilimo.

Kwa kima cha zaidi ya Euro Bilioni 34 bidhaa zilizosafirishwa nchi za nje mwaka uliopita zimefikia kima cha juu sana ambacho hakikuwahi kufikiwa kabla.

Kwahivyo, baada ya Marekani,Ufaransa na Hollamnd, Ujerumani imechukua sasa nafasi ya 4 kama muuzaji mkubwa wa mazao ya kilimo ulimwenguni.

Kiwanda cha ndugu Stolle kinafanya biashara ya nyama ya kuku na bata.Kila siku kiwanda chao kinachinja kuku 450.000 na bata 12.000 na kinatia mfukoni dala milioni 450 kwa mwaka.

Sehemu kubwa ya biashara ya kiwanda cha akina ‘GEBRÜDER STOLLE’ ya nyama ya kuku na bata imetawanyika katika matawi ya kampuni lao katika mikoa ya Lower Saxony,Mecklenburg-Vorpommern na mkoa wa Hessen.Nyama inayotayarishwa huko ni ya mchanganyiko ama ile iliochinjwa hapo hapo na kuuzwa au ile iliohifadhiwa barafuni na kuuzwa katika maduka -Supermärket ya mikoa hiyo.10% lakini ya nyama hiyo husafirishwa nchi za nje kama vile mkuu wa masoko wa kampuni Bw.Albert Focke anavpsimulia:

"Tunauza sana mashariki ya kati,tunasafirisha nyama Dubai na Oman ,takriban barabaarabu nzima,kwa sababu katika nchi hizo nyama nyingi ya kukuku au bata inapendwa."

Mwanzoni mwa miaka ya 1990 kiwanda chao cha nyama kilianza kusafirisha nyama nchi za nje na Bw.Focke anaeleza zaidi:

"Miaka 10 –12 hivi nyuma tulianza kusafirisha nchi za nje nyama kidogo.Awali ilikuwa kontaina moja kwa wiki na leo tunasafirisha hadi makontena 2 mpaka 3 kwa siku."-anaeleza Bw.Albert Focke-meneja wa soko.

Nyama kutoka Ujerumani inapendwa sana nchi za nje.Lakini pia mazao yanayotokana na maziwa.Na hasa chizi,kwani wakati huu imetia fora katika mazao yanayouzwa nchi za nje kutoka Ujerumani katika sekta ya kilimo.Mwaka jana 2004,viwanda vya kilimo na vya chakula vya Ujerumani vimeuuza mazao yao nchi za nje kuliko wakati wowote ule kabla.Vimeuza kiasi cha Euro bilioni 34,1 na ukilinganisha na mwaka uliotangulia huo ni muongezeko wa 6.4%.

Bidhaa zilizotengezwa Ujerumani au "MADE IN GERMANY" wakati huu zinaulizwa sana masokoni na wanunuzi.

Bibi Martina May ambae anahusika na uuzaji ngambo mazao ya kilimo katika Shirika kuu la Jumuiya ya wakulima ya Ujerumani (CMA) anaeleza:

"MADE IN GERMANY"-bidhaa zilizotengezwa Ujerumani zina heba na zinaangaliwa nchi za nje ni za sifa ya hali ya juu,zilizochunguzwa barabara uzuri wake na usalama wake kabla kuuzwa."

Wanunuzi wakubwa wa mazao ya kilimo kama hapo kabla wamesalia kuwa washirika wa asilia wa Ujerumani wa Umoja wa Ulaya na hasa Holland,Itali na Ufaransa ambao wananunua 75% ya mazao yote ya kilimo kutoka Ujerumani.Wanachama wapya wa Umoja wa Ulaya nao wanajiunga na safu hii kwani mazao yaliouzwa katika nchi hizo 2004 ziliongezeka kwa kima cha 12%.Masoko ya kuvutia mno mbali na Marekani ni Russia pia ambayo katika maonesho ya ‘wiki ya Kilimo’ wiki hii mjini Berlin, imekuja kama mtembezaji mkubwa wa mazao ya kilimo kutoka nje ya Ujerumani.China na nchi za mashariki ya kati pia kwavile zinapendelea sana mazao yanayotokana na maziwa.

Bibi Martina May wa shirika la soko la mazao la wakulima wa Ujerumani anasema zaidi,

"Huko kuna tabaka lenye nguvu la wanunuzi ,kuna tabaka la watu wapendao mno kusafiri nchi za nje ambao pia wameshafika Ulaya na ambao wanapenda pia kuonja tena vyakula vya kijerumani na kuna mazao ambayo hawayaoni madukani bali yanayokwenda viwandani kama malighafi kutengezewa mazao mengine. "

Hizo bidhaa kama chizi-inayotumiwa kama mali-ghafi katika viwanda vinavyotengeza vyakula vya haraka-haraka.Bei imepanda mno juu.

Hapo mwezi wa desemba ,mwaka uliomalizika hivi punde tani moja ya Mozzarella-inayopendwa mno kutiwa juu ya Pizza imefikia thamani ya dala 3000.Miaka 2 nyuma thamani yake ilikua dala 1900 kwa tani.Hata chizi za aina ya Edamer,Gouda na chizi nono,viwanda vya Ujerumani vinafanya biashara nzuri,kwani Holland,Itali na Wagiriki pekee hawawezi kulitosheleza soko kwa mahitaji .

Urusi haiagizi tu chizi bali hata nyama mbichi.Rumania na Ukraine halkadhalika,haziwezi kukidhi mahitaji yao.Hali hii lakini yaweza ikabadilika hara.Kwahivyo, bingwa huyu wa soko la nje Bibi Martina May anasisitiza kuwa ni muhimu kwa soko la bidhaa zilizokwisha tengezwa kutoka Ujerumani kupanuliwa.Kwani, viwanda vya mazao ya kilimo vya Ujerumani vinatupia macho tu nchi za nje.

Anasema zaidi bibi May kwamba, mbinyo wa mashindano ya kibiashara uliopo katika viwanda vya kutengezea vyakula jinsi ulivyo mkubwa nchini Ujerumani,hakuna nchi nyengine ya Ulaya inayoikaribia n a kila mtindo wa kuuza bidhaa kwa bei yoyote ile ya chini na kushindana kwa bei ukizidi ndipo itakavyozidi kwa viwanda kupigania masoko ya nje kuongeza pato na faida zao.

Katika viwanda vinavyotengeza vyakula viwango vya ukuaji biashara mwaka 2004 viliweza tu kufikiwa katika biashara ya n’gambo –export na sio kutoka soko la ndani ya nchi-asema bibi May.

Hata kampuni la Lower saxony la ndugu Stolle linalouza nyama ya kuku na bata ,halitaki asilani kuachana na biashara ya kuuza nchi za nje nyama yao.Nchi za kiarabu zinaununua sana nyama ya kukuku na bata ambayo kutokana na wezani wake mdogo au hafifu,haitakiwi sana na wachuuzi.Itakua hasara kubwa kwahivyo, kwa muujibu wa meneja wa meneja-masoko Albert Focke kulipoteza soko hilo la nje.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW