1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Susan Rice mshauri wa usalama wa taifa

6 Juni 2013

Rais Barack Obama, akiwapuuzia wakosoaji kutoka chama cha Republican, amemteua mwanadiplomasia Susan Rice kuwa mshauri wake wa masuala ya usalama wa taifa, na kumpa sauti kubwa katika sera za mambo ya kigeni.

WASHINGTON, DC - JUNE 05: U.S. President Barack Obama (2nd L) speaks as former aide Samantha Power (L), U.S. Ambassador to the United Nations Susan Rice (R) and incumbent National Security Adviser Tom Donilon (2nd R) react during a personnel announcement at the Rose Garden of the White House June 5, 2013 in Washington, DC. President Obama has nominated Rice to succeed Donilon to become the next National Security Adviser. Obama has also nominated Power to succeed Rice for her position to UN. (Photo by Alex Wong/Getty Images)
Rais Barack Obama akiwatambulisha Susan Rice (kulia) na Samantha Power (kushoto)Picha: Getty Images

Licha ya shutuma kuwa alitoa taarifa zisizo sahihi kwa taifa baada ya mashambulio mabaya dhidi ya raia wa Marekani mjini Benghazi, nchini Libya Rice anachukua wadhifa huo kutoka kwa mshauri anayeondoka madarakani Tom Donilon.

Uteuzi huo uliofanywa jana Jumatano(05.06.2013) , pamoja na uteuzi wa mwanaharakati wa kutetea haki za binadamu Samantha Power kuchukua nafasi inayoachwa wazi na Rice kama balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa , unaashiria hatua ya Obama kuwapendelea washauri ambao wana mwelekeo wa kupendelea uingiliaji kati zaidi wa Marekani nchi za nje kwa minajili ya kuchukua hatua za kibinadamu.

Susan RicePicha: picture-alliance/dpa

Obama hatarajiwi kubadilika

Lakini bado si wazi iwapo nadharia hiyo itabadilisha sera za rais Obama kuhusu Syria , ambako amezuwia mbinyo hadi sasa wa kutumia nguvu za kijeshi kuutatua mzozo wa nchi hiyo wa vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Uteuzi wa Rice unatoa unatoa nafasi ya kupumua kidogo baada ya uchunguzi wenye utata uliofanyika mjini Benghazi kulazimisha kutoweza kufikiriwa kuchukua wadhifa wa waziri wa mambo ya kigeni katika kipindi cha pili cha utawala wa Obama .

Samantha PowerPicha: picture alliance/AP Photo

Rais , ambaye alimtetea Rice kwa nguvu zote dhidi ya ukosoaji kutoka kwa wabunge wa chama cha Republican , amemsifu rafiki yake huyo wa karibu kwa kusema kuwa ni mzalendo halisi ambaye huweka maslahi ya nchi yake kwanza.

Wasifu

"Susan ni mtumishi halisi wa umma, ambaye huweka maslahi ya nchi yake mbele. Simuwoga na ni jasiri. Susan anatambua kuwa hakuna kitu mbadala kwa uongozi wa Marekani. Ni mwenye hamasa , na mtendaji. Na natambua kuwa Susan ni bingwa wa kweli wa kupigania haki na ubinadamu."

Lakini pia ni mtu mwenye kutambua kuwa tunapaswa kutumia nguvu zetu kwa busara na panapostahili.

Rice mwenye umri wa miaka 48 anachukua wadhifa huo wenye ushawishi mkubwa wa usalama wa taifa akiwa mtu wa karibu kabisa na rais kutoka kwa Tom Donilon , ambaye anaacha wadhifa huo mwezi Julai baada ya kutumikia kwa muda wa zaidi ya miaka mitano katika utawala wa rais Obamna.

Rais Barack Obama na rais wa China Xi JinpingPicha: Reuters

Mabadiliko katika ngazi ya juu ya kikosi cha utawala cha rais Obama yanakuja muda mfupi wakati akianza kupambana na agenda ya sera za mambo ya kigeni. Anatarajiwa kukutana na rais wa China Xi Jinping katika mkutano usio wa kawaida mjini Califonia kuanzia Ijumaa, na kisha atasafiri kwenda katika mataifa ya Ulaya na Afrika baadaye mwezi huu.

Mwandishi: Sekione Kitojo/ape

Mhariri: Mohammed Khelef

Ruka sehemu inayofuata Gundua zaidi
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW