Suu Kyi: ''Sina chuki na utawala wa kijeshi''.
14 Novemba 2010Katika hotuba yake ya kwanza baada ya zaidi ya miaka saba, aliwaambia maelfu ya wafuasi wake leo, kwamba anataka kufanya kazi pamoja na vyombo vyote vya kidemokrasia, ili kuweza kuboresha maisha ya watu Myanmar, ambayo ni moja ya nchi masikini kabisa kusini mashariki mwa Asia.
Jana Jumamosi viongozi wa nchi mbalimbali duniani walipongeza kuachiliwa huru kwa Suu Kyi, baada ya zaidi ya miaka 15 ya kifungo cha gerezani na nyumbani.
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel, amesema msimamo wa Suu Kyi wa kutopenda ghasia na wa kutokukata tamaa umemfanya apendwe na watu.
Nye Waziri wa Mambo ya nchi za Nje wa Ujerumani Guido Westerwelle ameutaka uongozi wa kijeshi nchini Myanmar kuchukua hatua zaidi.
Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban KI Moon, amemuelezea Suu Kyi kama kichocheo cha matumaini duniani.