Sweden, Ukraine zatinga Euro 2016
18 Novemba 2015Sweden ilitoka sare ya magoli 2-2 ugenini dhidi ya Denmark, na hivyo wakafanikiwa kufuzu baada ya kuushinda mchezo wa kwanza kwa mabao 2-0.
Mshambuliaji nyota Zlatan Ibrahimovic ndiye aliyefunga mabao yote mawili ya Sweden wakati ya Denmark, yakifungwa na Yussuf Poulsen na Jannik Vestergaard. Ukraine ilijikatia tikiti licha ya kutoka sare ya bao 1-1 na Slovenia. Katika mchezo wa kwanza Ukraine iliishinda Slovenia mabao 2-1.
Timu 24 zilizofuzu kushiriki michuano hiyo ya Ulaya kando na wenyeji Ufaransa ni:
Albania, Austria, Belgium, Croatia, Jamhuri ya Czech, England, Ufaransa, Ujerumani, Hungary, Iceland, Italia, Ireland ya Kaskazini, Poland, Ureno, Jamhuri ya Ireland, Romania, Urusi, Slovakia, Uhispania, Sweden, Uswisi, Uturuki, Ukraine, Wales
Mwandishi: Bruce Amani/AFP
Mhariri: Abdulrahman