Sydney. Afikishwa mahakama baada ya siku 12.
14 Julai 2007Matangazo
Polisi wa Australia wamemfikisha mahakamani daktari raia wa India, siku 12 baada ya kumkamata akihusishwa na jaribio lililoshindwa la shambulio la bomu katika gari nchini Uingereza.
Jeshi la polisi la Australia limesema Mohammed Haneef ameshtakiwa kwa kutoa msaada kwa kundi la kigaidi, kosi ambalo linahusika na adhabu ya kwenda jela miaka 15.