SYDNEY: Korea Kaskazini itoe madini yake ya plutonium
16 Oktoba 2007Matangazo
Mpatanishi mkuu wa Marekani kuhusu mradi wa nyuklia wa Korea ya Kaskazini,Christopher Hill,kwa mara nyingine tena ametoa mwito kwa nchi hiyo,kusalim madini yake ya plutonium.Marekani inaamini,Korea ya Kaskazini ina kiasi ya kilo 50 za plutonium.
Hill amesema,ingawa ni vigumu kutoa madini yake,hiyo lakini ni hatua nyingine iliyo muhimu katika utaratibu wa kusitisha mradi wake wa nyuklia.
Tume ya wataalamu wa kinyuklia ipo nchini Korea ya Kaskazini tangu juma lililopita,kubomoa mtambo mkuu wa nyuklia wa Korea ya Kaskazini.Mapema mwaka huu,Pyongyang ilikubali kuachilia mbali mradi wake wa nyuklia na badala yake inapewa misaada katika sekta ya nishati na masuala ya kisiasa.