1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Syria imeondowa wanajeshi wake toka Libnan,ripoti ya umoja wa mataifa yathibitisha

24 Mei 2005

Tume ya Umoja wa mataifa imethibitisha,Syria imewahamisha wanajeshi wake wote toka nchi jirani ya Libnan.Ripoti ya umoja wa mataifa imesema wakaguzi wa tume hiyo hawajagundua hata mwanajeshi mmoja wa Syria nchini Libnan.Mwishoni mwa mwezi uliopita,Syria ilisema imewarejesha nyumbani wanajeshi wake wote kutoka Libnan.Wakati huo huo wapiga kura milioni tatu wa Libnan wanajiandaa kwa uchaguzi wa bunge utakaoanza jumapili ijayo .Viongozi wa upande wa upinzani wa Druze na Maronite Walid Djumlat na jenerali wa zamani Michel Aoun wameshindwa kuafikiana juu ya orodha ya watetezi.Mvutano huo unatishia kuvuruga muungano wa upande wa upinzani ,muungano uliopatikana baada ya kuuliwa waziri mkuu wa zamani Rafik Hariri,february 14 iliyopita.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW