SiasaSyria
Syria na Israel kuanza awamu mpya ya mazungumzo
5 Januari 2026
Matangazo
Afisa aliyezungumza kwa sharti la kutotambulishwa kwa kuwa hakuwa na ruhusa ya kuzungumza hadharani, ameliambia shirika la habari la AP kwamba ujumbe kutoka Syria utaongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje Asaad al-Shibani na Mkuu wa Kurugenzi Kuu ya Ujasusi, Hussein Salameh.
Amesema, lengo kuu la Syria kwenye mazungumzo hayo ni kufufua tena makubaliano ya kujitenga ya mwaka 1974 yalioanzisha eneo la ulinzi linalodhibitiwa na Umoja wa Mataifa kusini mwa Syria na kuhakikisha vikosi vya Israel vilivyotwaa udhibiti wa eneo hilo la ulinzi zaidi ya mwaka mmoja uliopita vinaondolewa.
Hata hivyo, si maafisa wa Israel wala msemaji wa ujumbe wa Marekani nchini Syria Tom Barrack walikuwa tayari kuzungumzia hilo, walipoombwa kufanya hivyo.