1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSyria

Syria: Watu 21 wauwawa katika shambulizi la kundi la IS

8 Novemba 2023

Watu 21 wamekufa nchini Syria baada ya kundi la kigaidi linalojiita Dola la Kiislamu IS, kuwavamia wapiganaji wanaounga mkono na serikali.

Wapiaganaji wa kundi la Dola la Kiislam
Wapiaganaji wa kundi la Dola la KiislamPicha: Dabiq/Planet Pix via ZUMA Wire/ZUMAPRESS/picture alliance

Magaidi hao walifanya shambulizi la kuvizia katika kijiji cha al Kawm kilichopo kati ya mji wa Homs unaodhibitiwa na serikali na ule wa Raqqa unaodhibitiwa na vikosi vya Kikurdi vinavyoungwa mkono na Marekani.

Maafisa wa Syria hawakutoa tamko mara moja juu ya shambulio hilo, na kundi la IS halijadai kuhusika na shambulio hilo.

Shambulio hilo limetokea huku ghasia zikiongezekakatika maeneo mengine nchini Syria. 

Soma pia:Iran yasema wanachama 28 wa IS wakamatwa kutokana na njama ya kuishambulia Tehran

Kundi la wanamgambo wa Iraq wanaoungwa mkono na Iran huendesha mara kwa mara mashambulizi kwenye kambi za wanajeshi wa Marekani katika maeneo ya mashariki na kusini mwa Syria.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW