MigogoroSyria
Syria: Safari za ndege za kimataifa Damascus kuanza tena
4 Januari 2025Matangazo
Safari za aina hiyo za kibiashara zilikuwa zimesitishwa kufuatia kuondolewa madarakani kwa rais Bashar al-Assad mwezi uliopita. Shirika la habari la umma SANA limesema safari za kuingia na kutoka uwanja wa ndege wa kimataifa mjini Damascus zitaanza Jumanne wiki ijayo.
Likimnukuu mkuu wa Mamlaka ya Safari za Anga, shirika la SANA limesema serikali imeanza awamu ya kufanya matengenezo kwenye viwanja vya Aleppo na Damascus kwa msaada wa washirika wake ili viweze kuzikaribisha ndege kutoka kote ulimwenguni. Ndege za kimataifa za misaada na wajumbe wa kigeni wa kidiplomasia tayari wamekuwa wakitua nchini Syria. Safari za ndani za ndege pia zimerejea.