Syria yatumia manowari kupambana na wapinzani
15 Agosti 2011Matangazo
Kwa mujibu wa ripoti za mashahidi, mbali na vifaru na majeshi ya nchi kavu, sasa manowari zinatumiwa kushambulia maeneo yenye wakaazi wengi katika mji wa bandari wa Latakia.
Wanaharakati wa haki za binadamu wamesema, idadi kadhaa ya raia waliuawa katika mashambulio ya hapo jana. Ripoti za vyombo vya habari zinasema, kati ya watu 19 na 26 wameuawa. Wapinzani wa Assad wameamua kuendelea na maandamano yao, licha ya Latakia na miji mingine ya Syria kushambuliwa na majeshi ya serikali.