1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Taa yazimika kwenye gazeti la "News Of The World"

Abdu Said Mtullya8 Julai 2011

Historia ya miaka 168 ya gazeti maaruf "News Of The World"kufikia tamati jumapili ijayo!

Taa ya gazeti maaruf la Uingereza, News Of The World kuzimika jumapili ijayo.Picha: newsoftheworld.co.uk

Kurasa za Gazeti maaruf duniani , "News Of The World" lenye historia ya miaka 168 zitafungwa daima Jumapili ijayo. Hatua hiyo inafuatia kashfa ya kudakiza simu za watu mbalimbai kinyume na sheria. Habari juu ya gazeti hilo kufungwa jumapili ijayo ziliripuka kama bomu kwa wasomaji wake nchini Uingereza na duniani kote.

Shirika la habari la Uingereza Reuters limesema uamuzi wa kulifunga gazeti hilo ndilo jawabu lililotolewa kwa kashfa hiyo ya kudakiza mazungumzuo ya simu za watu. Kufungwa kwa gazeti la News Of The World ambalo ni gazeti ndugu la kila jumapili "The Sun", maana yake ni kwamba dunia inalipoteza gazeti lililokuwa na mauzo makubwa nchini Uingereza.

Jumapili ijayo ndiyo utakuwa mwisho wa historia ya miaka 168 ya gazeti hilo. Juu ya hayo Mwenyekiti wa uchapishaji bwana James Murdoch mtoto wa mmiliki , Rupert Murdoch ameeleza kuwa ni jambo la kusikitisha, kwake na kwa kampuni yake kwa gazeti hilo kufungwa.

Hatua ya kulifunga gezeti hilo kongwe "News Of The World" ilitangazwa katika njia ya kushangaza na mwenyekiti huyo bwana James Murdoch aliesema kuwa gazeti hilo wakati wote limekuwa linawakosoa wengine lakini lenyewe limeshindwa kujikosoa.

Hatua ya kulifunga gazeti hilo imefuatia baada ya kudhihirika kwamba watumishi wake walizidakiza simu za watu zaidi ya alfu nne ikiwa, pamoja na zile za wahanga wa uhalifu na wa mashambulio ya kigaidi. Wamiliki wa gazeti hilo wamesikitishwa juu ya uamuzi wa kufungwa kwa gazeti hilo lakini wamesema shughuli za kuzidakiza simu za watu ni tabaini ya maadili ya uandishi wa habari. Juu ya mkasa wa gazeti hilo Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron amesema leo kwamba kila kilichotokea kitachunguzwa.

Mwandishi/Stephan lochner/SWR/

AFP/

Tafsiri/Mtullya abdu/

Mhariri/Othman Miraj/


Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW