1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Taasisi ya GHF kufungua tena vituo vyake Gaza

5 Juni 2025

Taasisi ya GHF inayoendesha utoaji wa misaada katika Ukanda wa Gaza imefunga vituo vyake lakini imesema inapanga kuvifungua tena

Gazastreifen | Hilfslieferung der Gaza Humanitarian Foundation GHF
Picha: Gaza Humanitarian Foundation/REUTERS

Sababu ya Taasisi hiyo ya GHF, ya kuvifunga vituo vyake vya kugawa misaada huko Gaza, Taasisi hiyo, inayoungwa mkono na Marekani na Israel imesema ni kutokana na tahadhari iliyotolewa na jeshi la Israel kwamba barabara zinazoelekea kwenye vituo vya usambazaji wa misaada "zinazingatiwa kuwemo miongoni mwa maeneo ya mapigano".  

Msikiti ulioharibiwa katika mashambulizi ya Israel katika mji wa Deir al-Balah katika Ukanda wa GazaPicha: Ramadan Abed/REUTERS

Taasisi hiyo ilikuwa imepanga kufungua tena vituo vyake vya usambazaji wa misaada katika Ukanda wa Gaza siku ya Alhamisi, ingawa imesema huenda shughuli zake zinaweza kuchelewa kuanza hadi baadaye leo mchana baada ya vituo hivyo kufungwa siku ya Jumatano kwa sababu ya "kazi ya ukarabati."

Soma pia: Shambulizi la droni la Israel laua watu 12 Gaza

Wakati huo huo miili ya mateka wawili wa Israel ilipatikana wakati wa operesheni ya kijeshi katika Ukanda wa Gaza. Wahasiriwa wametambuliwa kama Gadi Haggai aliyekuwa na umri wa miaka 72 na mke wake Judih Weinstein aliyekuwa na miaka 70. Jeshi la Israel limeeleza kwamba miili ya mateka hao wawili ilipatikana katika eneo la Khan Younis, kusini mwa Gaza. Taarifa zaidi zinasema miili ya Haggai na mkewe imerudishwa katika eneo la Nir Oz nchini Israel, walikoishi wanandoa hao kwa ajili ya mazishi.

Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu amesema katika salamu zake za rambirambi kwa familia za mateka hao kwamba yeye na mkewe wamehuzunishwa mno na vifo vyao.

Hapa nchini Ujerumani, Waziri wa Mambo ya Nje Johann Wadephul anajiandaa kumkaribisha mwenzake wa Israel, Gideon Saar, mjini Berlin Alhamisi, wakati ambapo hali katika Ukanda wa Gaza ikisababisha wasiwasi ndani ya serikali ya Ujerumani.

Mawaziri hao wa Mambo ya Nje wa Ujerumani na Israel watalitembelea jumba la makumbusho ya Wayahudi waliouawawa Ulaya, karibu na lango la Brandenburg mjini Berlin ambako wataweka mashada ya maua.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Johann WadephulPicha: Kay Nietfeld/dpa/picture alliance

Mengineyo Shirika la ulinzi wa kiraia huko Gaza limesema mashambulizi ya Israel yamesababisha vifo vya takriban Wapalestina 10 hii huku jeshi likiendelea na mashambulizi makali.

Soma pia: GHF: Tunasitisha huduma kwa muda Gaza

Wakati huo huo, jamaa wa mateka wa Israel wanaoshikiliwa huko Gaza na wafuasi wao walikusanyika kwenye maandamano ya kila wiki katika mji wa Tel Aviv, wakitaka kusitishwa kwa mapigano na kufikiwa makubaliano ya kuwarejesha mateka waliosalia wanaozuiliwa huko Gaza.

Yehuda Cohen, baba wa mateka Nimrod Cohen, alitoa ombi kwa Rais Trump na mjumbe wake maalum Steve Witkoff. Amesema: "Kwako Rais Trump na mjumbe wako maalum Steve Witkoff. Tafadhali, naomba umlazimishe Netanyahu avimalize vita na kwenda kwenye meza ya mazungumzo kufikia makubaliano ya kuwaachilia mateka wote. Hii ndiyo njia pekee ya kumaliza mateso yote. Hii ndiyo njia pekee nitakayomuona mwanangu Nimrod akiwa hai."

Marekani siku ya Jumatano ilipiga kura ya turufu kupinga Azimio la Baraza Usalama la Umoja wa Mataifa lenye lengo la kupunguza vita vya Gaza, ikisema kwamba azimio hilo litawaimarisha wanamgambo wa Kipalestina wa kundi la Hamas.

Vyanzo: RTRE/DPA

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW