Taasisi ya Goethe nchini Kenya yafungua milango yake kwa umma
18 Juni 2010Matangazo
Taasisi ya Goethe jijini Nairobi Kenya leo inafungua milango yake kwa umma kwa lengo la kutoa habari kuhusu shughuli za idara zake tatu, zikiwemo idara ya utamaduni, idara ya maktaba na habari na idara ya lugha ya Kijerumani. Washiriki wengine kwenye shughuli hiyo ya leo ni shirika la Ujerumani linalohusika na mabadilishano ya wanafunzi, DAAD, ambalo litatoa taarifa kuhusu masomo ya juu nchini Ujerumani. Shule ya Kijerumani ya mjini Nairobi na idara ya lugha ya Kijerumani ya chuo kikuu cha Nairobi, pia zitawakilishwa leo katika taasisi ya Goethe.
Josephat Charo alipata fursa ya kuzungumza na msemaji wa taasisi ya Goethe mjini Nairobi, Bi Irene Bibi, ambaye kwanza alikuwa na haya ya kueleza.
Mwandishi: Josephat Charo
Mhariri: Othman Miraji