1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tahadhari yatolewa dhidi ya MONUSCO kuondoka haraka Kongo

29 Septemba 2023

Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa jana walielezea wasiwasi wao kufuatia wito wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wa kutaka kuharakisha zoezi la kuviondoa vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa.

DR Kongo MONUSCO
Serikali ya Kongo inataka vikosi vya walinda amani wa Umoja wa Mataifa, MONUSCO, viondoke mwaka huu badala ya Disemba mwaka 2024.Picha: MONUSCO/Xinhua/picture alliance

Wiki iliyopita, Rais wa Kongo Felix Tshisekedi alitoa wito kwa Umoja wa Mataifa kuharakisha zoezi la kuuondoa ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa, MONUSCO ambao umekuwa nchini humo kwa takribani miaka 25.

Tshisekedi amehimiza zoezi hilo lianze mwishoni mwa mwaka huu, badala ya Desemba 2024 kama ilivyopangwa.

Mwezi Desemba, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linatarajiwa kurefusha muda wa MONUSCO kuhudumu nchini Kongo, ingawa nchi hiyo imetilia shaka uwezo na ufanisi wa kikosi hicho kuwalinda raia katika kipindi cha miongo kadhaa ya ghasia za makundi ya wanamgambo wenye silaha.

     

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW