1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Taifa Stars kukipiga na Nigeria mechi ya kwanza AFCON

22 Desemba 2025

Ikumbukwe kuwa AFCON ya Morocco itakuwa mara ya nne kwa timu hiyo ya taifa ya Tanzania kushiriki michuano hiyo, baada ya kushiriki awali mwaka 1980, 2019 na 2023.

Fußball | Africa Cup of Nations | Tansania - Demokratische Republik Kongo
Timu ya taifa ya Tanzania ilipomenya na na DRC Kongo mwaka 2024 katika michuano ya AFCON 2023.Picha: Fadel SennaAFP/Getty Images

Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars kesho Disemba 23 itatupa karata yake ya kwanza dhidi ya Nigeria katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) inakayofanyika nchini Morocco

Taifa stars imepangwa kundi C lenye timu ya Uganda,Tunisia,na Nigeria

Ikumbukwe kuwa AFCON ya Morocco itakuwa mara ya nne kwa Taifa Stars kushiriki michuano hiyo, baada ya kushiriki awali mwaka 1980, 2019 na 2023. Hivyo, mchezo wa kesho dhidi ya Nigeria sio tu mwanzo wa mashindano, bali ni mwendelezo wa historia ya Tanzania katika jukwaa la soka la Afrika.

Lakini pamoja na kushiriki huko kwa mara tatu mfululizo,Taifa Stars haijawahi kupata ushindi katika mechi yeyote ya michuano hii ingawa pengine mara hii inaweza kupata ushindi huko Morocco.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW