1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Taiwan yajihadhari kufuatia jaribio la kombora la China

Josephat Charo
30 Septemba 2024

Wizara ya ulinzi ya Taiwan imesema usalama na maendelezo ya eneo la Indo-Pasifiki yanahusiana na maendeleo ya dunia na vitendo vyovyote vinavyotishia na kuleta uchochezi vinavuruga uthabiti wa kikanda.

Vikosi maalumu vya jeshi la wanamaji la Taiwan wakifanya luteka za kujilinda
Vikosi maalumu vya jeshi la wanamaji la Taiwan wakifanya luteka za kujilindaPicha: Patrick Aventurier/abaca/picture alliance

Taiwan imesema iko katika hali ya juu ya tahadhari baada ya kubaini ufyetuaji kadhaa wa makombora upande wa China bara, siku chache baada ya serikali ya mjini Beijing kufanya jaribio la kombora la masafa marefu linaloweza kuvuka bara moja hadi lingine.

Wizara ya ulnzi ya Taiwan imesema imegundua ufyetuaji huo wa makombora na kitengo cha ufyetuaji makombora cha China na jeshi katika mikoa na maeneo ya ndani ya Mongolia, Gansu, Qinghai na Xinjiang kuanzia saa moja kasoro dakika kumi Jumamosi iliyopita.

China ilifanya jaribio la kombora la masafa marefu Jumatano wiki iliyopita, likilifyetua katika bahari ya Pasifiki, katika jaribio lake la kwanza kabisa la aina hiyo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW