1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Taiwan yarekodi ndege 153 luteka ya kijeshi ya China

15 Oktoba 2024

Wizara ya Ulinzi ya Taiwan imesema imegundua ndege 153 za kijeshi za China zinazoshiriki katika mazoezi ya kijeshi kwenye kisiwa hicho.

Ndege za kivita za China zikishiriki mazoezi ya utayarifu wa kivita
Ndege za kivita za China zikishiriki mazoezi ya utayarifu wa kivitaPicha: Xi Bobo/Photoshot/picture alliance

Wizara hiyo imesema leo kuwa kati ya ndege zilizoonekena, 111 zilivuka eneo muhimu katika Ujia wa Taiwan ambao unazitenganisha China na Taiwan. 

Kulingana na wizara hiyo, meli 14 za jeshi la wanamaji la China pia zilionekana karibu na kisiwa hicho katika kipindi hicho. 

Soma pia:China yadhihirisha nguvu kubwa kwa kufanya mazoezi ya kivita karibu na Taiwan 

Waziri Mkuu wa Taiwan, Cho Jung-tai, amesema mazoezi hayo ya kijeshi hayaleti tu wasiwasi kwa Taiwan, lakini yanahatarisha kudhoofidha ukanda wote. 

Wakati huo huo, maelfu ya askari wa kikosi cha majini wa Marekani na Ufilipino wameanza mazoezi ya pamoja ya kijeshi ya siku 10 kaskazini na magharibi mwa Ufilipino, siku moja baada ya China kufanya mazoezi makubwa kuzunguka Taiwan.