1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChina

Taiwan yaitaka China kugawana majukumu ili kudumisha amani

1 Januari 2024

Kiongozi wa Taiwan Tsai Ing-wen ametoa wito kwa China kugawanya majukumu ya pamoja ili kudumisha amani na utulivu katika mlango bahari wa Taiwan na kanda hiyo, kulingana na makubaliano ya sasa ya jumuiya ya kimataifa

Kiongozi wa Taiwan Tsai Ing-wen akihutubia wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kitaifa mbele ya Jengo la Rais
Kiongozi wa Taiwan Tsai Ing-wenPicha: Chiang Ying-ying/AP/dpa/picture alliance

Wakati wa hotuba yake ya mwaka mpya, Tsai amesema kuwa ''wanatumai kwamba pande hizo mbili zitaanzisha tena mawasiliano thabiti haraka iwezekanavyo'' na kuongeza kuwa Taiwan pia inataka kwa pamoja kutafuta njia kwa pande hizo mbili kuishi kwa pamoja kwa kipindi kirefu kupitia kanuni za "amani, usawa, demokrasia na mazungumzo."

Soma pia: Taiwan yaripoti shughuli zaidi ya kijeshi za China huku uchaguzi ukikaribia

Tsai amesema kuwa chaguo la Taiwan katika siku zijazo bado ni kuendelea kudumisha demokrasia na kulinda amani.      

Wakati wa mkutano na waandishi wa habari, Tsai alisema kuwa mustakabali wa uhusiano kati ya Taiwan na China utaamuliwa kwa pamoja na watu wa Taiwan kupitia utaratibu wa kidemokrasia kwa sababu "Taiwan ni nchi ya kidemokrasia.''