1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaJapan

Takaichi kuibuka na ushindi mkubwa Japan - maoni

2 Februari 2026

Chama cha Waziri Mkuu wa Japan, Sanae Takaichi, kinatazamiwa kupata ushindi mkubwa kwenye uchaguzi wa wiki ijayo kwa mujibu wa uchunguzi wa maoni uliochapishwa jioni ya Jumapili (Februari 1).

Japan  2025 | Sanae Takaichi
Waziri Mkuu wa Japan, Sanae Takaichi, anatazamiwa kupata ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi wa Februari 8.Picha: Kohei Choji/AP Photo/picture alliance

Kwa mujibu wa matokeo ya uchunguzi yaliyochapishwa na gazeti mashuhuri la Asahi, chama hicho cha kiliberali kitajizolea viti 233 kati ya 465 vya bunge, likiwa ongezeko kubwa kutoka 198 kilivyonavyo sasa.

Pamoja na mshirika wake, chama cha Ishin, muungano wao unakisiwa kufikia viti 300.

Chama kikubwa cha upinzani, Reform Alliance, kinahofiwa kupoteza nusu ya viti vyake 167, kinavyovishikilia sasa.

Kwa sasa muungano wa Takaichi una wingi mdogo kwenye baraza la chini la bunge na umezidiwa nguvu kwenye baraza la juu.

Waziri mkuu huyo alitangaza kulivunja bunge mwezi uliopita na kuitisha uchaguzi mpya tarehe 8 Februari.

Thamani ya hatifungani za serikali ya Japan ziliripotiwa leo kupanda baada ya wawekezaji kupata matumaini ya Takaichi kurejea madarakani kuendeleza sera yake iliyojikita kwenye kukata matumizi na kodi kubwa. 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW