1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Takriban nyumba 2,750 zimechomwa moto DRC

Admin.WagnerD30 Julai 2024

Mgogoro wa kikabila jimboni Tanganyika umesababisha kuuawa kwa watu 3, na wanane wakijeruhiwa huku nyumba 2750 zikiteketezwa na watu wa kabila la watwa.

Tanzania Tanganjika Provinz
Moja kati ya nyumba zilizochomwa moto katika kijiji kimoja katika jimbo la Tanganyika DRC.Picha: Zuberi Ally/DW

Tukio hilo lilitokea Alfajiri ya Julai 29, na kusababisha watoto kutembeakilomita kadhaa kutafuta maeneo salama kunusuru maisha yao. DW ilifuka katika eneo la tukio umbali  wa kilomita 18 kusini mashariki mwa Kalemie na kujionea hali ilivyo.

Hali ya kufuka kwa moshi katika baadhi ya nyumba ndivyo vilivyopata nafasi kuwa katika eneo hilo. Mamia ya raia wakiwemo wanawake na watoto wamekimbia Kijiji hicho kwa kutembea kwa miguu kilomita nyingi wakielekea mji wa Kalemie na vijiji jirani.

Ombi kwa serikali ya Kongo kuwalinda raia

Raia wa Kongo, Mzete ya Makanisi (Mti Mawazo) akitoroka mapigano katika maeneo ya machafuko.Picha: Zuberi Ally/DW

Katika tukio hilo watu watatu akiwemo askari jeshi mmoja waliuwawa na wengine wanane walijeruhiwa kwa mishali. Tumbwe Mwamba Celestin ni kiongozi wa kijiji hicho ameitolea wito serikali kuimarisha  usalama

Shirika la kutetea raia NDSCI kupitia makamu kiongozi wao Byaesse Issa wameiomba serikali kurejesha usalama katika vijiji mbalimbali jimboni humo kwani matukio mengi yametokea mwezi huu

Chama Mukalay raia  mwenye huzuni ambae amekutwa amekaa mbele ya nyumba yake iliyoungua ameionyooshea kidole cha lawama serikali.

Serikali yataka wananchi warejee katika makazi yao

Waziri wa mambo ya ndani na ulinzi jimboni humuo Dieudonne Kasaka ambaye alikuwepo kwenye eneo la tukio, amethibitisha vifo vya watu hao na kuomba raia warejee katika kijiji hicho kwani ulinzi umehimarishwa

Raia wanaendelea kuwalaumu  askari jeshi kwa kile wanachosema ni kutokuwajibika ipasavyo kwenye matukio ya mara kwa mara kwenye Vijiji kadhaa. Jeshi la taifa FARDC jimboni Tanganyika kupitia msemaji wao John Munta wamedai  jumla ya nyumba 2750 zimeunguzwa na wamewaomba raia kuliamini jeshi hilo.

Soma zaidi: Rais Tshisekedi ana nadi sera zake Tanganyika

Rekodi zinaonesha kuwa watu takribani 10 wameuawa ndani ya siku zisizo zidi 15 huku 7 miongoni mwao wakiuwawa  kwa kuchinjwa katika vijiji vya Mutenta, na Tabac Congo.

DW kalemie

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW