1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wafungwa 150 wenye itikadi kali, wanashikiliwa Ujerumani

28 Februari 2018

Magereza ya Ujerumani yanajitahidi kukabiliana na wafungwa wenye itikadi kali

Türkei Gefängnis in Antalya
Picha: picture-alliance/dpa/T. Bozoglu

Idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka baada kufunguliwa kwa misururu ya uchunguzi unaohusiana na ugaidi katika miezi ya hivi karibuni.

Takriban Waislamu 150 wenye itikadi kali wanashikiliwa katika magereza ya Ujerumani, kwa mujibu wa takwimu za afisi ya Idara ya Upelelezi ya Serikali kuu ya Ujerumani zilizoschapishwa kwenye gazeti la kila siku nchini Ujerumani la Die Welt.

Gazeti hilo lililonukuu afisi ya Idara ya Upelelezi ya Serikali Kuu, linasema kuwa wanaume hao ama wanatumikia kifungo au wanatuhumiwa kwa makosa yanayohusiana na ugaidi.

wafungwa wanaishikiliwa walikuwa wapiganaji wa IS

Wapiganaji wa Dola la Kiislamu-ISPicha: Getty Images/AFP/G. Ourfalian

Gazeti hilo linaendelea kusema kuwa, watu kadhaa wanaohusishwa na ugaidi wanashikiliwa katika magereza hayo ambao huenda ni wafuasi wanawaunga mkono itakadi kali.

Waziri wa sheria wa jimbo la Hesse nchini Ujerumani Eve Kuöhene-Hö ameliambia gazeti hilo kuwa, katika miaka michache ijayo, Ujerumani italazimika kutarajia wafungwa wengi zaidi  wenye itikadi kali.

Ameendelea kusema kuwa, ``kuna uchunguzi unaoendelea dhidi ya mamia ya washukiwa. Uchunguzi huo unafanyika kote nchini Ujerumani wanaochunguzwa wengi wao wakiwa wapiganaji wa Kiislamu wanaorejea Ujerumani kutoka Mashariki ya Kati baada ya kuwa katika mapambano ya kulisaidia  kundi la Dola la Kiislamu.``

Kunhe-Hörmann ameonya kuwa idadi ya Waislamu wenye itikadi kali walioko kweye magerez ya ya Ujerumani ni ``changamoto kubwa ya kuvunja nguvu ugaidi pamoja na kuuzuia.``

Amesema  iwapo magereza hayatatumika kuwasaidia watu wenye itikadi kali kutangamana na jamii pana ``kuna hatari ya kuachia waislamu wenye itikadi kali katika jamii.``

Visa 1200 vya kigaidi vinachunguzwa

Wafungwa 150 wanazuliwa Ujerumani kwa itikadi kaliPicha: Getty Images/J. Moore

Mwezi Desemba, maafisa wa Ujerumani walikiri juu ya kuanzishwa uchunguzi mara tano zaidi dhidi ya ugaidi mwaka 2017 ikilinganishwa na miaka ya awali. Takriban visa 1200 vinavyochunguzwa vinahusu vitendo vya kigaidi na zaidi ya asilimia 80 ya visa hivyo vinahusiana na Waislamu wenye itikadi kali.

Vinajumuisha wahubiri wenye misimamo mikali, wauaji walioshindwa katika njama zao na wale wanaorejea kutoka Syria na Iraq ambako mapigano yanaendelea.

Gazeti la Die Welt, limekinukuu, Chama cha Maafisa wa Magereza wa Ujerumani kikisema kuwa idadi ya wafungwa wenye itikadi kali wanaongeza hatari kwa usalama kwa wafanyikazi, kabla ya kutoa wito wa kutolewa mafunzo zaidi.

Katika taifa jirani la Ufaransa, walinzi wa magereza walifaya maandamano mwezi uliopita , wakilalamikia ghasia katika magereza yalioyokuwa na idadi ya wafungwa kupita kiasi.

Maafisa wa magereza walisusia kazi baada ya mpiganaji wa Kiislamu kutoka Ujerumani alipomkata mlinzi wa gereza kwa kutumia mkasi.

Mwandishi: Shisia Wasilwa, Die Welt

Mhariri: Saumu Yusuf,