Migogoro
Wanafunzi 14 watekwa nyara na watu wenye silaha Nigeria
17 Aprili 2026
Matangazo
Kamishna wa polisi wa jimbo hilo Ifeanyi Emenari amesema vijana hao walitekwa nyara Alhamisi walipokuwa njiani wakisafiri kwa basi kuelekea katika mji wa Otukpo ambako mtihani wao ulipangwa kufanyika. Mamlaka za usalama nchini humo zimeanzisha msako wa kuwaokoa wanafunzi hao.
Wanamgambo waendelea kutishia usalama
Makundi ya wabeba silaha na wanamgambo wenye itikadi kali wamekuwa wakiwateka nyara wasafiri, wanafunzi na jamii za vijijini nchini Nigeria. Hadi sasa mamlaka hazijabaini waliohusika na hakuna kundi lolote lililokiri kuhusika na utekaji huo.