JamiiAsia
Takriban Warohingya 170 wamewasili Indonesia
2 Desemba 2023Matangazo
Mkuu wa mkoa wa jamii yenye kujikita na shughuli za uvuvi wa Aceh huko Indonesia, Miftah Cut Ade amesema Warohingya wapatao 170 wamewasili katika mipaka ya ardhi ya taifa hilo leo hii.
Kiongozi huyo amesema wengi wa watu hao waliowasili kwa boti kutoka Myanmar ni wanawake na watoto. Kwa miaka mingi, Warohingya wameondoka Myanmar yenye idadi kubwa ya watu wa madhehebu ya Budha ambapo kwa ujumla huchukuliwa kama wahamiaji wa kigeni kutoka Asia Kusini na hivyo kunyimwa haki ya uraia na manyanyaso mengine.
Takriban Warohingya milioni moja wanaishi katika kambi za wakimbizi kwenye wilaya ya mpakani ya Bangladeshi ya Cox's Bazar, wengi wao ni baada ya kutoroka ukandamizaji ulioongozwa na jeshi nchini Myanmar wa 2017.