1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Somalia:Takriban watu 100 wameuawa katika milipuko ya mabomu

30 Oktoba 2022

Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud amesema takriban watu 100 wameuawa katika mashambulio mawili ya mabomu ya kutegwa kwenye gari.

Somalia, Mogadischu | Bildungsministerium von zwei Explosionen getroffen
Picha: Farah Abdi Warsameh/AP/picture alliance

Tukio hilo liliendeshwa hapo jana katika mtaa wenye shughuli nyingi mjini Mogadishu. Kuliwahi kutokea shambulio katika eneo hilo miaka mitano iliyopita ambapo lori lililojazwa vilipuzi lilisababisha vifo vya zaidi ya watu 500.

Hassan Sheikh Mohamud, Rais wa SomaliaPicha: Farah Abdi Warsameh/AP/picture alliance

Rais Mohamud akiwa kwenye eneo kulikotokea milipuko hiyo, aliwaambia waandishi wa habari kuwa karibu watu wengine 300 walijeruhiwa huku akiwaomba washirika wa kimataifa kuwaagiza madaktari nchini humo na kusema hawawezi kuwasafirisha majeruhi wote nje ya nchi  kwa matibabu.

Wapiganaji wa kundi la al-Shabab nchini SomaliaPicha: picture alliance / AP Photo

Kundi la al-Shabab lenye mafungamano na al-Qaida ambalo hushambulia zaidi mji mkuu Mogadishu na ambalo linadhibiti eneo kubwa ya nchi hiyo, limedai kuhusika na shambulizi hilo na kusema lililenga ofisi za wizara ya elimu ambayo wametaja ni ngome ya maadui wanaopokea msaada kutoka katika nchi zisizo za kiislamu ili kuwaondoa watoto wa kisomali katika imani ya Kiislamu.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW