1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiNigeria

Watu 14 wameuawa na wengine 60 kutekwa nyara nchini Nigeria

25 Septemba 2023

Takriban watu 14 wameuawa na wengine 60 wametekwa nyara siku ya Jumapili na watu wenye silaha kaskazini magharibi mwa jimbo la Zamfara nchini Nigeria

Maafisa wa usalama washika doria katika jimbo la Zamfara nchini Nigeria huku watu wakiwasubiri wanafunzi wa Jangebe waliookolewa baada ya kutekwa nyara mnamo Machi 3 2021
Maafisa wa usalama washika doria katika jimbo la Zamfara nchini NigeriaPicha: Afolabi Sotunde/REUTERS

Tukio hilo limeripotiwa na wakazi wa eneo hilo pamoja na kiongozi wa kitamaduni, siku mbili baada ya watu wengine 12 kutekwa nyara katika chuo kikuu jimboni humo.

Watu wengine sita wauawa katika tukio tofauti nchini Nigeria

Katika tukio jingine kaskazini mashariki mwa Nigeria, watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa Kiislamu walivizia msafara wa magari uliokuwa ukisindikizwa na  jeshi, na kuwaua askari wawili na raia wanne. Shuhuda wa tukio hilo amesema washambuliaji walichoma moto magari matano na kuondoka na lori moja.

Soma pia:Wanafunzi 35 wa Chuo Kikuu watekwa nyara Nigeria

Zamfara ni mojawapo ya majimbo yaliyoathirika zaidi vitendo vya utekaji nyara vinavyoendeshwa na magenge ya uhalifu yenye silaha. Rais wa Nigeria Bola Tinubu bado hajaeleza ni jinsi gani atakavyoshughulikia hali iliyoenea ya ukosefu wa usalama.