1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaAsia

Takriban watu 15 wameuwawa kwa tetemeko la ardhi Afganistan

Hawa Bihoga
7 Oktoba 2023

Tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 6.3 katika kipimo cha Richter lililopiga Magharibi mwa Afganistan leo, limeuwa watu takriban 15 na wengine kadhaa kujeruhiwa.

Baadhi ya raia wakiwa katika taharuki baada ya tetemeko
Baadhi ya raia wakiwa katika taharuki baada ya tetemekoPicha: Mashal/Xinhua/IMAGO

Maafisa katika idara ya kupambana na majanga nchini humo wanasema huenda idadi ya vifo ikaongezeka baada ya ripoti ya maporomoko na waathiriwa kukwama kwenye majengo yalioanguka kufuatia tetemeko hilo.

Soma pia:Tetemeko la ukubwa wa 6.3 lapiga Magharibi mwa Afganistan

Msemaji wa Mamlaka ya Kitaifa ya Kudhibiti Majanga Mullah Jan Sayeq amesema "takriban watu 40 wamejeruhiwa." huku akisisiza kuwa hiyo ni taarifa ya awali huenda idadi ikaongezeka.  Huduma muhimu ikiwemo mawasiliano ya simu katika eneo hilo zimetatizika.


Itakumbukwa kuwa, mwezi Juni mwaka uliopita zaidi ya watu 1,000walikufa na maelfu waliachwa bila makaazi baada ya tetemeko la ukubwa wa 5.9 ambalo ni baya zaidi nchini humo kwa kipindi cha robo karne kupiga jimbo masikini la Paktika. 
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW