1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan

Watu 18 wamekufa kufuatia kuzuka tena kwa mapigano Sudan

12 Juni 2023

Takriban watu 18 wamekufa kufuatia kuzuka tena kwa mapigano makali nchini Sudan mara tu baada ya kumalizika kwa muda wa makubaliano wa usitishaji mapigano wa saa 24

Sudan | Unruhe in Khartoum
Picha: AP

Waandishi wa habari wameripoti mashambulizi ya anga na makabiliano kati ya jeshi na vikosi vya RSF. Mwandishi wa habari wa Kanada mwenye makao yake mjini Cairo kufuatia matukio katika nchi jirani ya Sudan, ameiambia DW kuwa vurugu zimekuwa zikiendelea katika baadhi ya mikoa.

Marekani na Saudi Arabia zalaani mapigano 

Marekani na Saudi Arabia ambao wamekuwa wapatanishi katika mzozo huo wamelaani vikali kitendo cha kuzuka tena kwa vurugu. Mzozo huo ulioanza April 15 tayari umesababisha vifo vya mamia ya watu na kuwalazimu wengine zaidi ya milioni 1.9 kuyahama makazi yao.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW