Takriban watu 18 wauawa kwenye shambulizi la RSF, Sudan
17 Septemba 2025
Matangazo
Vyanzo hivyo pia vimesema idadi ya watu isiyojulikana wanaaminika kuzikwa hasa katika eneo la kusini la kambi ya wakimbizi ya Abu Shouk, viungani mwa mji huo.
Kundi moja la wanaharakati, moja kati ya mamia ya makundi yanayoorodhesha maasi yanayofanyika katika vita hivyo, limesema wapiganaji wa RSF wamekuwa wakisonga mbele tangu Jumatatu kutoka kaskazini mwa mji huo ambapo mashambulizi yanaendelea.
Kundi hilo limesema raia kadhaa waliuawa majumbani mwao na wengine kuwekwa kizuizini chini ya mazingira ya kutatanisha.
Pia limeripoti kutokea kwa mapigano makali, mashambulizi na kuendelea kuwepo kwa droni katika anga ya El-Fasher kwa siku ya pili mfululizo.