SiasaKazakhstan
Takriban watu 28 waokolewa wakiwa hai katika ajali ya ndege
25 Desemba 2024Matangazo
Shughuli za uokoaji zinaendelea, huku mamlaka zikitangaza kuwa kati ya watu waliokufa kwenye ajali hiyo ni pamoja na marubani wa ndege hiyo. Shirika la habari la serikali la nchini Azerbaijan, Azertag limeripoti kuwa abiria 62 na wafanyakazi watano walikuwa ndani ya ndege hiyo aina ya Embraer 190. Ndege hiyo ilikuwa ikisafiri kutoka mji mkuu wa Azerbaijan, Baku kuelekea Grozny, ambao ni mji mkuu wa Jamhuri ya Urusi ya Chechnya. Uwanja wa ndege wa Grozny uliripotiwa kufungwa kwa sababu ya ukungu, hali iliyoifanya ndege hiyo kushindwa kutua kwenye uwanja huo na hivyo rubani akajaribu kutua katika uwanja wa Makhachkala, katika mji mkuu wa mkoa wa Dagestan ambako ndege hiyo iligongana na kundi la ndege na kusababisha ajali hiyo.