1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Takriban watu 30 wauwawa Lebanon kwa mashambulizi ya Israel

Angela Mdungu
10 Novemba 2024

Wizara ya afya ya Lebanon imesema kuwa watu wasiopungua 30 wameuwawa katika mashambulizi ya anga yaliyofanywa na jeshi la Israel kwenye maeneo kadhaa nchini humo.

Mashambulizi ya anga yameendelea kutikisa maeneo kadhaa ya Lebanon
Shughuli za uokoaji zikifanyika katika kijiji cha Aalmat baada ya mashambulizi ya anga ya IsraelPicha: Hassan Ammar/AP/picture alliance

Mji wa Aalmat in Jbeil umeripotiwa kuwa na vifo vingi kati ya hivyo ambapo takriban watu 23 wameuwawa wakiwemo watoto saba. Wizara hiyo imeongeza kuwa idadi ya vifo huenda ikaongezeka wakati vipande vya miili ya watu  vikiwa vimefukuliwa kutoka eneo la tukio kwa ajili ya kutambuliwa.

Soma zaidi: 

Shambulio jingIsrael yaendeleza mashambulizi yake Gaza na Lebanonine lililokilenga kituo cha afya kwenye mji wa Adlon kusini mwa Lebanon limewauwa watu watatu. Wizara ya afya ya Lebanon imesema watu wengine wanne waliuwawa kwenye mashambulizi a anga ya Israel Jumamosi katika eneo la Beqaa magharibi huko mashariki mwa Lebanon.

Wakati huohuo, Viongozi wa nchi za Kiarabu na za Kiislamu wameanza kuwasili Saudi Arabia kwa ajili ya mkutano utakaojadili vita vya Israel huko Gaza na Lebanon.  Mkutano huo utakaoanza Jumatatu ulitangazwa na Saudia mwishoni mwa Oktoba wakati wa mkutano wa muungano wa kimataifa unaoshinikiza kuundwa suluhisho la katika mzozo wa Israel na Palestina.