1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN: Watu 50,000 waikimbia Myanmar kufuatia mapigano

10 Novemba 2023

Umoja wa Mataifa umesema takriban watu 50,000 wameyakimbia makaazi yao kaskazini mwa Myanmar kwa sababu ya mapigano ya muungano wa makundi ya kikabila yenye silaha ulioanzisha mashambulizi dhidi ya jeshi.

Myanmar | Raketenabschuss von einer Militärbasis in der Stadt Lashio
Picha: AFP/Getty Images

Mapigano hayo yaliyoanza wiki mbili zilizopita yameendelea katika jimbo la kaskazini la Shan karibu na mpaka wa China, katika kile wachambuzi wanasema kinaleta changamoto kubwa zaidi kwa utawala wa kijeshi tangu uliponyakua mamlaka mwaka 2021.

Kundi linalojiita Muungano wa kidemokrasia wa kitaifa wa jeshi la Myanmar (MNDAA), lile linalojiita Jeshi la Ukombozi la Ta’ang (TNLA) na jingine la Jeshi la Arakan (AA) yamesema yamekamata makumi ya vituo vya kijeshi na kuziba njia muhimu za biashara kuelekea China.

Kiongozi wa Myanmar asema uasi unatishia kulisambaratisha taifa hilo

Kulingana na ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoratibu masuala ya kibinadamu (OCHA), kufikia jana Novemba 9, karibu watu 50,000 kaskazini mwa Shan, walilazimika kuyahama makaazi yao.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW