Watu 518 waliuwawa katika ghasia za uchaguzi Tanzania
23 Aprili 2026
Matangazo
Ripoti iliyowasilishwa Alhamisi na Mwenyekiti wa tume hiyo Jaji Mohamed Chande Othman imesema zaidi ya watu 800 walijeruhiwa kwa risasi. Jaji Chande amesema idadi ya vifo huenda ikawa kubwa zaidi kwa sababu baadhi ya familia ziliwazika wapendwa wao bila kuwapeleka kwenye vyumba vya kuhifadhi maiti.
Rais Samia kufanyia kazi mapendekezo ya tume
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hasan amejibu kuwa ameyapokea mapendekezo ya tume hiyo na atayafanyia kazi.
Tanzania ilikumbwa na ghasia hizo wakati wa uchaguzi baada ya vijana kuingia barabarani wakiishutumu serikali kwa kuunkandamiza upinzani. Tume hiyo imesema maandamano hayo hayakuwa ya amani, yaliratibiwa, na imetaka uchunguzi zaidi kuhusu matumizi ya silaha.