1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu milioni 4.4 kutoka Ukraine wana hadhi ya ulinzi Ulaya

Josephat Charo
11 Machi 2026

Ofisi ya takwimu ya Umoja wa Ulaya Eurostat imeripoti kwamba jumla ya raia milioni 4.38 wasio raia wa Umoja wa Ulaya waliokimbia Ukraine walikuwa na hadhi ya ulinzi wa muda katika Umoja wa Ulaya Januari 31 mwaka huu.

Ujerumani inaongoza kwa kuwahifadhi idadi ya wakimbizi wa Ukraine katika Umoja wa Ulaya
Ujerumani inaongoza kwa kuwahifadhi idadi ya wakimbizi wa Ukraine katika Umoja wa UlayaPicha: Carsten Koall/AFP

Ripoti iliyochapisha jana Jumanne inaonesha takwimu hiyo iliongezeka kwa 23,110, au asilimia 0.5 ikilinganishwa na mwisho wa mwezi Desemba 2025.

Nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya zinazohifadhi idadi kubwa zaidi ya wanufaika wa ulinzi wa muda kutoka Ukraineni Ujerumani yenye milioni 1.26, Poland yenye 956,990 na Jamhuri ya Czech yenye 397,185.

Wakimbizi wengi wa Ukraine wanaruhusiwa kufanya kazi katika nchi za Umoja wa Ulaya na pia kupokea fedha za kijamii na huduma za matibabu bila kulazimika kuomba hifadhi.

Umoja wa Ulaya umeongeza muda wa hatua hizi hadi Machi 2027, na mawaziri wa mambo ya ndani kwa sasa wanajadili kurefusha muda zaidi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW