1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiPakistan

Watu 12 wafariki kwa tetemeko la ardhi Pakistan

22 Machi 2023

Watu wasiopungua 12 wamefariki nchini Afghanistan na Pakistan, kufuatia tetemeko kubwa la ardhi lililotokea usiku na ambalo watu walilihisi umbali wa maelfu ya kilomita.

Pakistan Erdbeben 2005
Picha: Farooq Naeem/AFP via Getty Images

Miongoni mwa waliofariki, tisa, wameripotiwa kufa kaskazini magharibi mwa Pakistan, ambako zaidi ya majengo 10 yaliporomoka.

Hayo ni kulingana na idara inayoshughulikia majanga nchini Pakistan. Zaidi ya watu 100 wameripotiwa kujeruhiwa kufuatia tetemeko hilo.

Idara inayofuatilia matetemeko ya ardhi ya Marekani, imesema tetemeko hilo lilikuwa la ukubwa wa 6.5 kwenye vipimo vya Ritcha na kwamba kitovu chake ni eneo la Jurm, kaskazini mashariki mwa Afghanistan.

Tetemeko hilo lilidumu kwa muda wa sekunde 30.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW